Jumatano, 29 Januari 2014

HARUSI YA KANA (Wedding in Cana of Galilee)*sehemu ya tatu*

Na Mtumishi Gasper Madumla.
BWANA YESU ASIFIWE...
Haleluya...,
Natumaini utaitikia “ AMEN”
Karibu tule pamoja chakula hiki cha uzima,ikiwa leo ni siku ya tatu ya fundisho hili na ikiwa ndio mara yako ya kwanza kujifunza fundisho hili,basi bado hujachelewa maana sehemu zilizopita zote zinapatikana mahali hapa hapa.
Msingi wa fundisho hili umesimama katika Yoh.2:1-11.Na siku ya leo tunaendelea pale tulipoishia,tunasoma ;

“ Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.”Yoh.2:6

Haleluya…

Kwa taratibu za Kiyahudi,kulikuwa na mabalasi ya Kutawadha,
Neno “ kutawadha ” lina maana ya kujitakasa ( purification).Hivyo Mabalasi ni vyombo vilivyokuwa vikitumika kwa shughuli ya kujitakasa tu,na wala sio shughuli nyingine iwayo yote.
Tena Mabalasi ( waterpots of stone) ni vyombo maalumu vilivyotengenezwa kwa mawe safi ( according to the manner of purification of the Jews)
Mabalasi haya yalikuwa ni makubwa,ukubwa wa balasi moja ulikuwa ni madumu thelathini (thirty gallons apiece.),Say 30 peaces of gallons.

Sasa sikia;
Bwana Yesu anawaambia wakayajaze mabalasi maji.
(Kumbuka balasi moja lilikuwa madumu 30,)Kwa lugha nyingine Bwana Yesu alikuwa akiwaambia wakalete madumu 180 kwa mabalasi sita,ili kuyajaza maji mabalasi hayo yote.
Sasa pata picha hiyo,hata kama hujaambiwa ujazo wa dumu(gallon) moja ni wa lita ngapi,lakini chukulia kwamba yanahitajika madumu mia moja na themanini (180) ili mabalasi sita yajae maji,na ili muujiza utendeke.

Haleluya…

Wana wa Mungu,ifike wakati tusomapo Biblia tusichukulie kwa wepesi juu ya mazingira ambayo tunayoyasoma kama mfano huu wa harusi ya Kana,maana waweza ukaona kwamba ilikuwa ni rahisi kwa muujiza huu kutokea.

Hivyo utaona haikuwa rahisi,maana hawa wanafunzi hawakuenda harusini kwa ajili ya kuteka maji madumu mia moja na themanini(180) bali walikwenda kusherekea .
Pata picha,unafikiri ilikuwaje?

Yamkini walichafuka baada ya kubeba yale maji,maana maji walioambiwa wayateke yalikuwa ni mengi kiujazo.
Laiti kama ungelikuwa wewe,upo harusini na suti yako safi,smart,gafla mtu mmoja anakutuma wewe na wenzako wachache mkalete magallons 180,myajaze mapipa maji,Je si ungemkasilikia mtu huyo? Labda ungemwambia hivi;
“ Unajua nitachafuka ndugu,kama ni muujiza wataka kuufanya,basi si uufanye tu,kwani ni lazima mpaka tuchafuke kwa kuchota maji mengi hivyo...?

Nataka upate picha hiyo,maana hata wanafunzi wa Bwana Yesu nao vile vile walikuwa wamependeza,sababu nao walienda harusini.Tena ngoja nikuambie, kipindi kile ndio mazingira yalikuwa magumu sana maana wanafunzi hawa walikuwa wakivaa kanzu,sasa pata picha mtu aliyevaa kanzu huku akiwa anateka maji,ni tofauti kabisa na mtu atekaye maji huku akiwa amevaa suruali kama ilivyo siku hizi.

Oooh…,
Jina la Bwana lisifiwe mahali hapa…
Nampenda Yesu wa Nazareti…

Hivyo wanafunzi wake Bwana Yesu walishiriki kwa sehemu fulani katika muujiza wa Bwana Yesu wa kwanza wa kubadilisha maji kuwa divai.Sababu Wanafunzi ndio walioteka maji,naye Bwana Yesu akayageuza yale maji kuwa divai.
Jambo moja la msingi hapo tunalojifunza ni;
UTAYARI WA NDANI KWA KUANZA NA MOJA,MBILI NI YA BWANA.

Ninaposema utayari wa ndani wa kuanza na moja..Nina maana kwamba; Mungu hufanya jambo/MUUJIZA katika kanuni yake ya IMANI ambayo wewe unayefanyiwa muujiza huo ni lazima kwanza ufungue moyo wako,kwa kuamini kwamba Bwana anaweza,hiyo ni moja ambayo ni ya kwako wewe kama wewe.

“ …MBILI NI YA BWANA ” Hapa nina maana hii;
Ukishafungua moyo wako,kile kinachobakia cha kutendewa ni muujiza ambao ni kazi ya Bwana,na ndio maana nasema“mbili ni ya Bwana”

Mfano;
Chukulia unataka kuendesha gari ndogo ya gia(manual),yaani unataka kwenda mbele-Inakubidi uweke gia namba moja ili gari ianze kusogea,ile gia namba moja ya gari kusogea ni ya kwako,
lakini baada ya kusogea na kutaka gari ichanganye mwendo inakubidi ubadilishe gia,sasa kule kubadilisha gia,
katika suala la kiimani ni kazi ya Bwana,maana gia namba moja ni ya kukuonesha ;
NIA,UTAYARI wa kutaka kuondoka,lakini namna ya kuchanganya mwendo,sio kazi yako bali ni kazi ya Bwana na huo ndio mfano wa muujiza wa harusi ya Kana.
Yesu alihitaji utayari wa kuteka maji kwanza,kisha namna ya maji kuwa divai,ilikuwa ni kazi yake Yeye Bwana Yesu….

ITAENDELEA…

• Kwa huduma ya maombezi;
0655-111149.

UBARIKIWE.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Slider

Sample Text

Text Widget

HARUSI YA KANA (Wedding in Cana of Galilee)*sehemu ya tatu*

Jumatano, 29 Januari 2014 Leave a Comment

0 maoni »

Leave your response!

Sample Text

Contact

Slider

Racing

Travel

Cute

Videos

Popular Posts

My Place

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

Design by NewWpThemes | Blogger Theme by Lasantha - Premium Blogger Themes | New Blogger Themes