Jumamosi, 26 Oktoba 2013

RAIS WA BUNGE LA USWISI AELEZEA MABILIONI, MAGAZETI DAR KUFUNGIWA

Rais wa Bunge la Uswisi, Maya Graf (wa nne kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wa magazeti ya Mwananchi na The Citizen katika mahojiano maalumu, jijini Dar es Salaam. PICHA | EMMANUEL HERMAN

Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd kupitia magazeti yake ya Mwananchi na The Citizen, yalipata fursa pekee ya kumuhoji Rais Maya Graf, kuhusiana na masuala mbalimbali ikiwamo madhumuni ya safari yake, mabilioni hayo, uwazi wa mishahara ya viongozi wa juu serikalini na uhuru wa vyombo vya habari. Mwandishi wetu, Noor Shija alikuwa mmoja wa walioshiriki kufanya mahojiano na kiongozi huyo wa kitaifa na yafuatayo ni mahojiano hayo:

Jumamosi, 12 Oktoba 2013

WIZARA YA HABARI YAKOROGANA ,NIKUHUSU MAHABASU YA MAGAZETI.

Msomaji wa Gazeti la Mwananchi akiburudika na gazeti hilo mara baada ya kuanza shughuli za uchapaji wa gazeti, kumekuwepo na sintofahamu katika Wizara ya habari ya kutoa taarifa elekezi zinazo kinzana kuhusu kufungiwa kwa gazeti la Mwananch na Mtanzania. Picha na Fidelis Felix.

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla, jana alitoa taarifa kwa umma akieleza bayana kwamba yeye ndiye aliyeliruhusu gazeti hili kuendelea kutolewa kwa njia ya mtandao (online) na Gazeti la Rai kutolewa kila siku.

Makalla alitoa ufafanuzi huo muda mfupi baada ya Idara ya Habari-Maelezo kutoa taarifa kwamba Serikali imesikitishwa na Gazeti la Mwananchi na gazeti dada la Rai, Mtanzania kukiuka masharti ya adhabu walizopewa.

Septemba 27, mwaka huu Serikali iliyafungia Mwananchi kwa siku 14 na Mtanzania siku 90.

Wakati likianza kutumikia adhabu yake, Mwananchi ambalo tayari limemaliza kuitumikia, liliendelea kutoa taarifa kwenye tovuti yake wakati Kampuni ya New Habari (2006) Ltd ambayo inamiliki Mtanzania ilianza kuchapisha kila siku gazeti la Rai ambalo awali lilikuwa likichapishwa kila wiki.

Jumapili, 6 Oktoba 2013

makala :HAKUNA UGUMU WA KURUDI MISRI

Ndugu zangu,

Yanayotokea katika nchi yetu kwa sasa yanatutaka tufikiri kwa bidii. Kama nchi kuna safari tumeifunga. Na tulivyo Waafrika, tu mahodari wa kufunga safari, lakini si mahodari wa kupanga safari. Kufunga na kupanga safari ni vitu viwili tofauti.

Ndugu zangu,

Ni vigumu leo kwa Wana wa Israel kuamua kurudi tena Misri, hata kama, pamoja na chawa na kunguni walioaacha Misri, bado, kuna wanaokumbuka samaki na masufuria ya pilau waliyoayaacha Misri. Lakini, kijamii, na kwa kuingalia jamii yetu hii ilikotoka, ilipo sasa na inakoelekea, na tuone sasa, kuwa hakuna ugumu wa kurudi tena Misri. Na hapa nitazungumzia umuhimu wa sisi WaTanzania kujitambua.

Nahofia, kuwa moja ya kiini ya haya yanayotukuta sasa ni dhambi ya Ubaguzi iliyoanza kututafuna pole pole. Taratibu tunapoteza uwezo wetu wa kujitambua. Ni ukweli sasa, kuwa Watanzania hatujitambui, na kibaya zaidi, baadhi ya viongozi wetu wa kisiasa na kidini wanapoonyesha wazi wazi kuwa hawajitambui.

Maana, tumeanza sasa kuzungumza lugha za ' Wao Wakristo' na ' Sisi Waislamu'. Tunasahau, kuwa sisi ni ndugu wa damu. Kuwa SISI ni Watanzania Kwanza. Na lililo la kwanza kwetu ni ' Nchi Yetu' na maslahi yake.

Hii ni Nchi Yetu Sote. Kila Mtanzania kwa nafasi yake ana lazima ya kupigania Usalama wa Taifa letu. Usalama wa Nchi Yetu tuliyozaliwa. Hatuwezi kuilinda na kuijenga Nchi Yetu kwenye mazingira ya kubaguana. Kwenye mazingira ya kugawanyika kwa misingi ya udini, ukabila na rangi. Na hapa nitamrejea tena Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere na dhana ya Ujenzi wa Umoja wa Kitaifa.

Ni Mwalimu Nyerere aliyeuanzisha na kuusimamia mradi mkubwa wa Ujenzi wa Umoja wa Kitaifa, hata hivyo, tunaona sasa unavyoporomoka na kuliacha taifa letu mashakani. Ndio, Mwalimu alijenga misingi imara ya Ujenzi wa Umoja Wa Kitaifa ( Nation Building).

Kuijenga jamii ya Watanzania yenye kuamini kwenye ukweli kuwa sisi sote ni ndugu. Kwamba Nchi yetu haina dini. Yenye kupiga vita ubaguzi wa aina zote, iwe wa rangi, kabila au dini. Ilimchukua Mwalimu na taifa letu miaka mingi sana kuijenga misingi hiyo iliyowawezesha pia Watanzania kuwa na mioyo ya uzalendo kwa Taifa lao.

Tunaona sasa, kazi hiyo iliyochukua miaka mingi, kutokana na ubinafsi na uroho wa madaraka ya baadhi ya wanasiasa wetu, wanapelekea kubomoka kwa misingi hiyo na kuliacha taifa letu kwenye hatari ya kuangamia.

Ndio, msingi wake ni ubaguzi wa kisiasa unaotokana na ubinafsi na tamaa ya mali kwa baadhi ya tuliowapa dhamana za kufanya maamuzi makubwa kwa niaba yetu. Ni hali ya baadhi ya tuliowapa dhamana za uongozi kuishiwa chembe chembe za uzalendo; mapenzi kwa nchi yao.Ni watu wenye kulinda maslahi yao na ya wanaowazunguka. Wako tayari hata kutumia mbinu za Umafia kutimiza malengo yao. Kuna Watanzania wengi sasa wanaopoteza mioyo ya uzalendo kwa nchi yao.

Kuna hata wenye kufikia kutamka; 'Nchi hii ina wenyewe'. Kuna anayetamka hilo kwa lengo la kumtishia mwenzake au kulazimisha kitu fulani kifanyike. Lakini, kuna wenye kutamka hivyo kuashiria kukata tamaa. Kuwa hata wafanye nini, hakuna anayewasikiliza ama kuwajali. Hizi si dalili njema kwa taifa. Kuna wanaoiba mali ya umma mchana wa jua kali. Hakuna anayewagusa.

Ukiuliza utajibiwa; "Ah! Nchi ina wenyewe!". Kwamba kuna baadhi yetu hawajisikii kuguswa na nchi hii, hawajisikii kuwa na nguvu ya kupiga vita maovu yanayotusumbua. Baadhi yetu wameanza kupungukiwa na mapenzi na nchi yao.

Juni 16, 2004 nilipata kuandika hili kwenye gazeti la Majira; kuwa Tanzania ina vyote, kasoro Watanzania. Niliandika; kuwa Tanzania ni nchi nzuri sana. Ni nchi ya kujivunia. Kwamba Tanzania ni nchi kubwa sana kwa eneo. Ni nchi yenye rasilimali nyingi; ardhi yenye rutuba, mito, maziwa, milima, mabonde, bahari na vivutio vingi vya asili.

Hata hivyo, Tanzania ni moja ya nchi masikini sana duniani. Kwa nini? Ndio, kikubwa kinachokosekana Tanzania ni Watanzania. Tanzania tunayoijenga sasa ni mkusanyiko tu wa watu wa makundi mbali mbali wenye kwenda kwa staili ya 'kila mtu na lwake'. Idadi ya Watanzania wenye uzalendo na mapenzi kwa nchi yao inazidi kupungua. Ubinafsi umekithiri, na ubinafsi mbaya zaidi ni ule wenye kufanywa na viongozi.

Ndugu zangu, Hakuna ugumu wa kurudi Misri. Tuna lazima ya kupanga safari ya kurudi tena Misri. Inawezekana.

Ni Neno la Leo.

Maggid Mjengwa,

Iringa.
0754 678 252

Slider

Sample Text

Text Widget

RAIS WA BUNGE LA USWISI AELEZEA MABILIONI, MAGAZETI DAR KUFUNGIWA

Jumamosi, 26 Oktoba 2013 0 maoni

Rais wa Bunge la Uswisi, Maya Graf (wa nne kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wa magazeti ya Mwananchi na The Citizen katika mahojiano maalumu, jijini Dar es Salaam. PICHA | EMMANUEL HERMAN

Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd kupitia magazeti yake ya Mwananchi na The Citizen, yalipata fursa pekee ya kumuhoji Rais Maya Graf, kuhusiana na masuala mbalimbali ikiwamo madhumuni ya safari yake, mabilioni hayo, uwazi wa mishahara ya viongozi wa juu serikalini na uhuru wa vyombo vya habari. Mwandishi wetu, Noor Shija alikuwa mmoja wa walioshiriki kufanya mahojiano na kiongozi huyo wa kitaifa na yafuatayo ni mahojiano hayo: Read the full story

WIZARA YA HABARI YAKOROGANA ,NIKUHUSU MAHABASU YA MAGAZETI.

Jumamosi, 12 Oktoba 2013 0 maoni

Msomaji wa Gazeti la Mwananchi akiburudika na gazeti hilo mara baada ya kuanza shughuli za uchapaji wa gazeti, kumekuwepo na sintofahamu katika Wizara ya habari ya kutoa taarifa elekezi zinazo kinzana kuhusu kufungiwa kwa gazeti la Mwananch na Mtanzania. Picha na Fidelis Felix.

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla, jana alitoa taarifa kwa umma akieleza bayana kwamba yeye ndiye aliyeliruhusu gazeti hili kuendelea kutolewa kwa njia ya mtandao (online) na Gazeti la Rai kutolewa kila siku.

Makalla alitoa ufafanuzi huo muda mfupi baada ya Idara ya Habari-Maelezo kutoa taarifa kwamba Serikali imesikitishwa na Gazeti la Mwananchi na gazeti dada la Rai, Mtanzania kukiuka masharti ya adhabu walizopewa.

Septemba 27, mwaka huu Serikali iliyafungia Mwananchi kwa siku 14 na Mtanzania siku 90.

Wakati likianza kutumikia adhabu yake, Mwananchi ambalo tayari limemaliza kuitumikia, liliendelea kutoa taarifa kwenye tovuti yake wakati Kampuni ya New Habari (2006) Ltd ambayo inamiliki Mtanzania ilianza kuchapisha kila siku gazeti la Rai ambalo awali lilikuwa likichapishwa kila wiki. Read the full story

NI WAKATI WA UKOMBOZI KWA BARA LA AFIKA,HOTU HIYO KUTOLEWA NA MWANAHARAKATI OSCAR SAMBA.

Read the full story

makala :HAKUNA UGUMU WA KURUDI MISRI

Jumapili, 6 Oktoba 2013 0 maoni

Ndugu zangu,

Yanayotokea katika nchi yetu kwa sasa yanatutaka tufikiri kwa bidii. Kama nchi kuna safari tumeifunga. Na tulivyo Waafrika, tu mahodari wa kufunga safari, lakini si mahodari wa kupanga safari. Kufunga na kupanga safari ni vitu viwili tofauti.

Ndugu zangu,

Ni vigumu leo kwa Wana wa Israel kuamua kurudi tena Misri, hata kama, pamoja na chawa na kunguni walioaacha Misri, bado, kuna wanaokumbuka samaki na masufuria ya pilau waliyoayaacha Misri. Lakini, kijamii, na kwa kuingalia jamii yetu hii ilikotoka, ilipo sasa na inakoelekea, na tuone sasa, kuwa hakuna ugumu wa kurudi tena Misri. Na hapa nitazungumzia umuhimu wa sisi WaTanzania kujitambua.

Nahofia, kuwa moja ya kiini ya haya yanayotukuta sasa ni dhambi ya Ubaguzi iliyoanza kututafuna pole pole. Taratibu tunapoteza uwezo wetu wa kujitambua. Ni ukweli sasa, kuwa Watanzania hatujitambui, na kibaya zaidi, baadhi ya viongozi wetu wa kisiasa na kidini wanapoonyesha wazi wazi kuwa hawajitambui.

Maana, tumeanza sasa kuzungumza lugha za ' Wao Wakristo' na ' Sisi Waislamu'. Tunasahau, kuwa sisi ni ndugu wa damu. Kuwa SISI ni Watanzania Kwanza. Na lililo la kwanza kwetu ni ' Nchi Yetu' na maslahi yake.

Hii ni Nchi Yetu Sote. Kila Mtanzania kwa nafasi yake ana lazima ya kupigania Usalama wa Taifa letu. Usalama wa Nchi Yetu tuliyozaliwa. Hatuwezi kuilinda na kuijenga Nchi Yetu kwenye mazingira ya kubaguana. Kwenye mazingira ya kugawanyika kwa misingi ya udini, ukabila na rangi. Na hapa nitamrejea tena Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere na dhana ya Ujenzi wa Umoja wa Kitaifa.

Ni Mwalimu Nyerere aliyeuanzisha na kuusimamia mradi mkubwa wa Ujenzi wa Umoja wa Kitaifa, hata hivyo, tunaona sasa unavyoporomoka na kuliacha taifa letu mashakani. Ndio, Mwalimu alijenga misingi imara ya Ujenzi wa Umoja Wa Kitaifa ( Nation Building).

Kuijenga jamii ya Watanzania yenye kuamini kwenye ukweli kuwa sisi sote ni ndugu. Kwamba Nchi yetu haina dini. Yenye kupiga vita ubaguzi wa aina zote, iwe wa rangi, kabila au dini. Ilimchukua Mwalimu na taifa letu miaka mingi sana kuijenga misingi hiyo iliyowawezesha pia Watanzania kuwa na mioyo ya uzalendo kwa Taifa lao.

Tunaona sasa, kazi hiyo iliyochukua miaka mingi, kutokana na ubinafsi na uroho wa madaraka ya baadhi ya wanasiasa wetu, wanapelekea kubomoka kwa misingi hiyo na kuliacha taifa letu kwenye hatari ya kuangamia.

Ndio, msingi wake ni ubaguzi wa kisiasa unaotokana na ubinafsi na tamaa ya mali kwa baadhi ya tuliowapa dhamana za kufanya maamuzi makubwa kwa niaba yetu. Ni hali ya baadhi ya tuliowapa dhamana za uongozi kuishiwa chembe chembe za uzalendo; mapenzi kwa nchi yao.Ni watu wenye kulinda maslahi yao na ya wanaowazunguka. Wako tayari hata kutumia mbinu za Umafia kutimiza malengo yao. Kuna Watanzania wengi sasa wanaopoteza mioyo ya uzalendo kwa nchi yao.

Kuna hata wenye kufikia kutamka; 'Nchi hii ina wenyewe'. Kuna anayetamka hilo kwa lengo la kumtishia mwenzake au kulazimisha kitu fulani kifanyike. Lakini, kuna wenye kutamka hivyo kuashiria kukata tamaa. Kuwa hata wafanye nini, hakuna anayewasikiliza ama kuwajali. Hizi si dalili njema kwa taifa. Kuna wanaoiba mali ya umma mchana wa jua kali. Hakuna anayewagusa.

Ukiuliza utajibiwa; "Ah! Nchi ina wenyewe!". Kwamba kuna baadhi yetu hawajisikii kuguswa na nchi hii, hawajisikii kuwa na nguvu ya kupiga vita maovu yanayotusumbua. Baadhi yetu wameanza kupungukiwa na mapenzi na nchi yao.

Juni 16, 2004 nilipata kuandika hili kwenye gazeti la Majira; kuwa Tanzania ina vyote, kasoro Watanzania. Niliandika; kuwa Tanzania ni nchi nzuri sana. Ni nchi ya kujivunia. Kwamba Tanzania ni nchi kubwa sana kwa eneo. Ni nchi yenye rasilimali nyingi; ardhi yenye rutuba, mito, maziwa, milima, mabonde, bahari na vivutio vingi vya asili.

Hata hivyo, Tanzania ni moja ya nchi masikini sana duniani. Kwa nini? Ndio, kikubwa kinachokosekana Tanzania ni Watanzania. Tanzania tunayoijenga sasa ni mkusanyiko tu wa watu wa makundi mbali mbali wenye kwenda kwa staili ya 'kila mtu na lwake'. Idadi ya Watanzania wenye uzalendo na mapenzi kwa nchi yao inazidi kupungua. Ubinafsi umekithiri, na ubinafsi mbaya zaidi ni ule wenye kufanywa na viongozi.

Ndugu zangu, Hakuna ugumu wa kurudi Misri. Tuna lazima ya kupanga safari ya kurudi tena Misri. Inawezekana.

Ni Neno la Leo.

Maggid Mjengwa,

Iringa.
0754 678 252 Read the full story

Sample Text

Contact

Slider

Racing

Travel

Cute

Videos

Popular Posts

My Place

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

Design by NewWpThemes | Blogger Theme by Lasantha - Premium Blogger Themes | New Blogger Themes