Jumamosi, 26 Oktoba 2013

RAIS WA BUNGE LA USWISI AELEZEA MABILIONI, MAGAZETI DAR KUFUNGIWA

Rais wa Bunge la Uswisi, Maya Graf (wa nne kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wa magazeti ya Mwananchi na The Citizen katika mahojiano maalumu, jijini Dar es Salaam. PICHA | EMMANUEL HERMAN

Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd kupitia magazeti yake ya Mwananchi na The Citizen, yalipata fursa pekee ya kumuhoji Rais Maya Graf, kuhusiana na masuala mbalimbali ikiwamo madhumuni ya safari yake, mabilioni hayo, uwazi wa mishahara ya viongozi wa juu serikalini na uhuru wa vyombo vya habari. Mwandishi wetu, Noor Shija alikuwa mmoja wa walioshiriki kufanya mahojiano na kiongozi huyo wa kitaifa na yafuatayo ni mahojiano hayo:

Swali: Nini madhumuni ya safari yako na hii ni mara yako ya kwanza kutembelea Afrika na hasa Tanzania?

Jibu: Hii siyo mara yangu ya kwanza kutembelea Afrika, mara ya kwanza kuja Afrika ilikuwa mwaka 2011, nilitembelea nchi ya Senegal. Lakini kwa Tanzania ni mara yangu ya kwanza na kwa wadhifa wangu wa Rais naruhusiwa kusafiri nje ya nchi.(P.T)

Na mimi nilichagua Tanzania kwa sababu ya uhusiano mzuri kati ya Uswisi na Tanzania uliodumu kwa miaka mingi. Kuna raia wengi wa Uswisi wanaoishi Tanzania, pia tunasaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile hospitali ya Ifakara (Morogoro), ambayo nimeitembelea.

Pia tunashiriki katika uendelezaji wa miradi mingine mbalimbali kama vile sekta ya kilimo, makazi na masuala mengine yanayohusiana na Serikali. Nikiwa Rais wa Bunge ni muhimu kwangu kuthibitisha fedha tunazosaidia Tanzania kama zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Swali: Ulikutana na Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda. Mazungumzo yenu yalilenga maeneo gani na nini matokeo ya mkutano wenu?

Jibu: Kwanza nilifurahi kuonana na Spika, kwa kuwa sote ni wanawake katika nafasi ya uongozi unaofanana, mazungumzo yetu yaliegemea sana kuhusu nafasi za wanawake katika uwakilishi wa uongozi wa kisiasa.

Tulizungumza kuhusu kanuni na taratibu za mabunge yetu, pia tulizungumza kuhusu changamoto tunazokabiliana nazo.

Pia tulizungumza kuhusu idadi ya wanawake ndani ya Bunge na umuhimu wa wanawake kushika nafasi za uongozi katika sekta ya elimu, sekta ya uchumi na katika ngazi za juu za uongozi. Hayo ndiyo tuliyozungumza.

Swali: Nchi yako imekuwa na uhusiano wa muda mrefu na Afrika, na hasa Tanzania katika masuala ya Bunge, diplomasia na misaada ya maendeleo. Kwa kifupi unaweza kuelezea uhusiano wa masuala ya Bunge na hasa katika kubadilishana uzoefu?

Jibu: Tuna uhusiano wa muda mrefu hasa katika ngazi ya kibunge, tumekuwa tukifanya kazi pamoja katika masuala ya umoja ya kibunge (Inter-Parliamentary Union-IPU), ambapo *fanyika Geneva, Uswisi, hivi karibuni Anne Makinda alihudhuria, lakini hatukubahatika kuonana.

Masuala mengine ni kama vile misaada ya kimaendeleo ambayo imeimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Uswisi, mfano miradi iliyopo Dodoma na Ifakara (Morogoro).

Swali: Walipakodi wa Uswisi wamekuwa wakichangia juhudi za maendeleo ya Tanzania katika kupambana na umaskini kupitia nyanja za maendeleo ya kiuchumi, utawala bora, afya, maji na masuala ya jenda. Uwazi na rushwa ni mijadala iliyotawala Bunge letu, ni uzoefu upi unaoweza kutolewa kati ya nchi hizi mbili kuhakikisha utawala bora na vita dhidi ya rushwa?

Jibu: Kwanza napenda kuweka sawa kuwa suala hili nitalizungumzia hasa kwa upande wa Uswisi, na sitaweza kutoa maoni yoyote kwa upande wa Tanzania.

Kutokana na taratibu na kanuni za Bunge la Uswisi, nina wajibu kwa Serikali yangu, pia nina wajibu kwa Bunge. Tumekuwa tukitoa taarifa za uwajibikaji wa Serikali wa ngazi zote na wananchi wana haki ya kupata taarifa wanazozitaka kuhusiana na utendaji wa Serikali yao kwa ngazi zote.

[Balozi wa Uswisi nchini, Olivier Chave, aliingilia kati na kufafanua kuwa; kila mwananchi anayetaka taarifa kuhusu Serikali yake, ana haki kwa mujibu wa Katiba kupata taarifa hizo.]

Hata hivyo, Rais Graf aliendelea kutoa maelezo kuwa ni muhimu kuwapa taarifa wananchi ambazo kwa kiasi kikubwa zinahamasisha kuwapo kwa uhuru wa kutoa maoni, akisema: "Jana (Jumanne) tulitembelea TMF (Tanzania Media Fund) ambao tunawasaidia. TMF tunawafadhili na hasa katika kuboresha uandishi wa habari."

Ni muhimu pia kuwa na taasisi zisizo za kiserikali na taasisi za kijamii zenye nguvu zinazoweza kuaminika na kusimamia uwajibikaji.

Swali: Uswisi inaridhishwa na namna Tanzania inavyotumia misaada yake?

Jibu: Napenda kusema kuwa Uswisi imekuwa ikisaidia nchi nyingi na msaada wake kwa Tanzania uko kwenye miradi mbalimbali ambayo fedha hupitia kwenye bajeti ya serikali. Ni vizuri kuwa na udhibiti mzuri katika kuendeleza miradi hiyo. Na hii ni moja ya sababu za mimi kuwapo Tanzania kwa ajili ya kuangalia miradi ambayo tunasaidia.

Hapo likaulizwa swali la nyongeza lililotaka kufahamu maoni ya Uswisi kuhusu uamuzi wa Serikali ya Tanzania kufungia magazeti mawili, Mwananchi na Mtanzania.

Jibu: Kwa hili nitazungumzia kwa upande wa nchi yangu ambako ndiko nawajibika. Nakumbuka tukio la kufungia gazeti lilitokea wakati wa Vita vya Pili vya Dunia (vilivyopiganwa mwaka 1939 hadi 1945), tangu wakati huo hakuna utaratibu wala sheria ya kufungia vyombo vya habari.

Hapo tena Balozi Chave alifafanua zaidi kwamba; nimeulizwa sana suala hili, ninachoweza kusema ni kwamba Uswisi hatuna sheria ya kufungia magazeti au vyombo vya habari. Kama kuna mtu au Serikali wataona hawakutendewa haki na chombo cha habari, kwa kuchafuliwa au namna yoyote, mlalamikaji anatakiwa kwenda mahakamani ambako ndiko haki inapatikana. Serikali ikikosewa na chombo cha habari itaenda mahakamani kama mlalamikaji.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Slider

Sample Text

Text Widget

RAIS WA BUNGE LA USWISI AELEZEA MABILIONI, MAGAZETI DAR KUFUNGIWA

Jumamosi, 26 Oktoba 2013 Leave a Comment

0 maoni »

Leave your response!

Sample Text

Contact

Slider

Racing

Travel

Cute

Videos

Popular Posts

My Place

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

Design by NewWpThemes | Blogger Theme by Lasantha - Premium Blogger Themes | New Blogger Themes